Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:28

Vita vya Israel kwa Hamas ni kupandikiza chuki kwa vizazi; anasema Josep Borrell


Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell.
Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell.

Borrell ni miongoni mwa maafisa wa nchi za Magharibi ambao wamekosoa idadi ya raia waliouawa Gaza.

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell amesema kuwa jinsi Israel inavyoendesha vita vyake dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza ni “kupandikiza chuki kwa vizazi”.

Borrell alizungumza kabla ya mazungumzo tofauti ya mawaziri wa EU ambayo wanafanya leo Jumatatu, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli, Israel Katz na mwanadiplomasia wa juu wa Mamlaka ya Palestina, Riyad al-Maliki.

“Tunazo katika fikra zetu Hamas ni kina nani, kile Hamas imefanya, na kwa hakika tunapinga na tunalaani,” Borell aliwaambia waandishi wa habari. “Lakini amani na utulivu haviwezi kujengwa tu kwa njia za kijeshi, na sio kwa njia hii ya kutumia hatua za jeshi.”

Borrell ni miongoni mwa maafisa wa nchi za Magharibi ambao wamekosoa idadi ya raia waliouawa Gaza. Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza inasema Wapalestina angalau 25,105 wameuawa, wengi wao ni wanawake na watoto. Wizara hiyo haijataja idadi ya raia na wapiganaji wa Hamas miongoni mwa waliouawa.

Forum

XS
SM
MD
LG