Changamoto ya kutafuta fedha zaidi kwa ajili ya Ukraine wakati inapambana na maendeleo mapya katika maeneo ya uvamizi wa Russia, baada ya zaidi ya miaka miwili ya vita imetawala mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka nchi tajiri zaidi zenye kidemokrasia duniani katika mji wa Stresa, kaskazini mwa Italia.
Mkutano huo unafanyika wakati Kyiv, imesema imesimamisha operesheni za kusonga mbele dhidi ya Russia, katika mkoa wa Kharkiv lakini Jenerali mkuu wa Ukraine alikiri Jumamosi kwamba adui wao ana mafanikio kiasi na kusema mapambano yanaendelea.
Rais Volodymyr Zelenskyy, wa Ukraine ameongeza maombi ya msaada zaidi huku jeshi lake likihangaika.
Forum