Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:52

Waziri wa fedha wa Marekani aonya juu ya tishio la Israel kufunga njia za ufadhili kwa benki za Palestina


Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akifanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa G7 katika mji wa Stresa, Italy, Mei 23. Picha ya Reuters
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen akifanya mkutano na waandishi wa habari kabla ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa G7 katika mji wa Stresa, Italy, Mei 23. Picha ya Reuters

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen Alhamisi ameonya juu ya hatari ya “mzozo wa kibinadamu” ikiwa Israel itafunga njia muhimu ya ufadhili kwa benki za Palestina.

“Nina wasiwasi sana na tishio la Israel kuchukua hatua ambayo itasababisha benki za Palestina kutoruhusiwa kufanya biashara na benki za Israel,” aliwaambia waandishi wa habari katika mji wa kaskazini mwa Italy wa Stressa, ambako mawaziri wa fedha wa G7 wanakutana.

“Hizi njia za Benki ni muhimu kwa kutuma na kupokea pesa ambazo zinaruhusu uagizaji wa bidhaa kutoka Israel zenye thamani ya dola bilioni 8 kwa mwaka, ikiwemo umeme, maji, mafuta, na chakula, kadhalika kurahisisha mauzo ya nje yenye thamani ya dola bilioni 2 kwa mwaka ambayo Wapalestina wanategemea kwa maisha yao.”

Alipoulizwa nini Marekani na kundi la G7 wanaweza kufanya kukabiliana na tishio hilo, Yellen alisema alimwandikia waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu miezi kadhaa iliyopita kuhusu hali ya kiuchumi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Forum

XS
SM
MD
LG