Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:55

Umoja wa Ulaya wakamilisha maelezo kuhusu vikwazo vipya dhidi ya Russia


Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Majenerali Valery Gerasimov huko Rostov-on-Don, Russia. Picha na REUTERS
Rais wa Russia Vladimir Putin akizungumza na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu na Mkuu wa Majenerali Valery Gerasimov huko Rostov-on-Don, Russia. Picha na REUTERS

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wanakamilisha "maelezo ya mwisho" ya pendekezo la 12 la vikwazo dhidi ya Russia ambavyo vitajumuisha marufuku ya almasi, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema siku ya Jumatatu.

Borrell alisema Tume ya Ulaya, mtendaji mkuu wa EU, wanaweza kuidhinisha mpango uliopendekezwa siku ya Jumatano. Kisha utapelekwa katika Baraza la Umoja wa Ulaya, linalojumuisha nchi wanachama 27, kwa ajili ya kujadiliwa na kuidhinishwa.

Tangu uvamizi wa Russia nchini Ukraine uanze Februari 2022, EU tayari impetitisha vikwazo 11 dhidi ya Moscow ili kupunguza uwezo wa Kremlin wa kufadhili vita. Vikwazo hivyo vitagusa sekta zote na zinajumuisha baadhi ya watu na taasisi 1,800.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya waliliiambia shirika la habari la Reuters wiki iliyopita kuwa jumuiya hiyo yenye nchi 27 ilikuwa ikisubiri taa ya kijani ya G7 ili kusonga mbele na kuweka kizuizi cha Almasi.

Afisa wa EU alisema muda uliopo wa pendekezo la Tume ya Ulaya kwa mpango huo wa vikwazo, utajadiliwa na serikali 27 za EU, utakuwa "mapema wiki ijayo".

"Tunakamilisha maelezo ya mwisho ya mpango huu," Borrell alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG