Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:30

Mabehewa ya nafaka yaongezeka katika bandari za Ukraine


Mkaguzi anakagua uharibifu katika bandari ya nafaka baada ya shambulio lililoripotiwa kuwa la ndege za kijeshi za Russia huko Odesa, Agosti 2, 2023. Picha na REUTERS
Mkaguzi anakagua uharibifu katika bandari ya nafaka baada ya shambulio lililoripotiwa kuwa la ndege za kijeshi za Russia huko Odesa, Agosti 2, 2023. Picha na REUTERS

Idadi ya mabehewa yanayoelekea katika bandari kwenye mkoa wa Odesa nchini Ukraine yaliendelea kuongezeka katika kipindi cha wiki iliyopita kutokana na ufanisi wa uendeshaji wa njia mbadala ya usafirishaji wa nafaka nje ya Black sea, afisa mkuu wa shirika la reli alisema siku ya Alhamisi.

Valeriy Tkachov, Naibu mkurugenzi wa idara ya biashara katika Shirika la Reli la Ukraine, alisema kupitia ukurasa wa Facebook kwamba katika wiki iliyopita idadi ya mabehewa ya nafaka yaliyoelekea bandari za Odesa yaliongezeka kwa zaidi ya asilimia 26 kutoka 4,227 hadi kufikia 5,341.

Alisema hadi mabehewa 970 yamekuwa yakishusha nafaka kwenye ghala katika bandari hizo kila siku.

Wiki moja kabla idadi ya magari iliongezeka kwa karibu asilimia 50. Mwezi Agosti, Ukraine ilizindua "nji ya kibinadamu" kwa meli zinazoelekea katika masoko ya Afrika na Asia ili kujaribu kukwepa kizuizi kilichopo katika bahari ya Black sea, baada ya Russia kujitoa katika makubaliano ambayo yalikuwa yakiihakikishia Kyiv usafirishaji nje wa nafaka kwa njia ya bahari wakati wa vita.

Baadaye, afisa mwandamizi wa kilimo alisema njia hiyo - ambayo inapita katika pwani ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Black sea iliyoko Ukraine, kuingia katika eneo la bahari la Romania na kwenda hadi Uturuki - pia itatumika kwa usafirishaji wa nafaka.

Naibu Waziri Mkuu Oleksandr Kubrakov alisema Alhamisi meli 91 zilisafirisha tani milioni 3.3 za bidhaa za kilimo na chuma tangu ukanda huo uanze kufanya kazi mwezi Agosti.

Forum

XS
SM
MD
LG