Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:38

Mkuu wa EU atembelea Ukraine na kuwatuza wafanyakazi wa reli


Mkuu wa Umoja wa Ulaya ,Ursula von der Leyen, akizungumza na wanahabari mjini Kyiv, Ukraine Novemba 4, 2023.
Mkuu wa Umoja wa Ulaya ,Ursula von der Leyen, akizungumza na wanahabari mjini Kyiv, Ukraine Novemba 4, 2023.

Mkuu wa Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, amewasili kwenye mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv Jumamosi, na kukaribishwa na Rais Volodymr Zelenskyy.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, muda mfupi baada ya kuwasili, Von der Leyen aliongoza hafla ya kuwatuza wafanyakazi wa serikali kutoka shirika la reli la Ukraine. Von der Leyen amewapongeza akisema kwamba wamefanya kazi bila kuchoka, kwenye mazingira magumu tangu kuanza kwa uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine.

Ameongeza kuandika kwenye mtandao wa X uliyojulikana kama Twitter kwamba mazungumzo yake wakati wa ziara hiyo ambayo ni ya 6 nchini Ukraine, yataangazia mpango wa taifa hilo kujiunga na EU, pamoja na namna ya kuwajibisha Russia kutokana na ukatili wake.

Forum

XS
SM
MD
LG