Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:08

Njia mbadala ya usafirishaji bidhaa kutoka Ukraine inafanyakazi mbali na shambulio la Russia


UKRAINE-CRISIS/ATTACK-VESSEL
UKRAINE-CRISIS/ATTACK-VESSEL

Ukanda mbadala wa usafirishaji ulioko katika bahari ya Black Sea nchini Ukraine unafanya kazi licha ya shambulio la hivi karibuni la Russia dhidi ya meli ya raia, Naibu Waziri Mkuu Oleksandr Kubrakov alisema siku ya Alhamisi.

Maafisa wa Ukraine walisema siku ya Jumatano kombora la Russia liliharibu meli ya raia iliyokuwa na bendera ya Liberia iliyokuwa ikiingia katika bandari ya Black Sea katika mkoa wa Odesa, na kuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine wanne.

Meli hiyo ilitakiwa kusafirisha madini ya chuma kwenda China.

"Ukanda wa Ukraine: usafiri wa meli unaendelea kwa pande zote zinazotoka na kwenda kwenye bandari katika mkoa wa Big Odesa," Kubrakov alisema kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Alisema kuwa meli sita zilizokuwa na tani 231,000 za mazao ya kilimo zimeondoka bandarini ndani ya mkoa wa Odesa na kuelekea Mlango wa Bahari wa Bosphorus nchini Uturuki.

"Meli tano zinasubiri kuingia bandarini kupakia mizigo. Msururu kwenye ukanda wa Ukraine uliendelea licha ya mashambulizi ya kimfumo ya Russia kwenye miundombinu ya bandari," Kubrakov aliongeza.

Baada ya kujiondoa katika makubaliano ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha usafirishaji salama wa nafaka kutoka Ukraine kupitia Black Sea, Russia imekuwa ikishambulia mara kwa mara miundombinu ya bandari za Ukraine. Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG