Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:32

Blinken asema ushirikiano kati ya Russia na Korea Kaskazini unatia wasi wasi


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amekemea kile alichosema kuwa, “mwenendo hatari,” wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Korea Kaskazini na Russia, kufuatia ripoti kwamba Pyongyang inatoa silaha kwa Moscow kwa ajili ya vita vya Ukraine.

“Hiyo ni hatua ya kutia wasi wasi kwetu pamoja na mataifa mengine kote ulimwenguni,” amesema Blinken wakati akihutubia wanahabari mjini Seoul, muda mfupi baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini, Park Jin. Idara ya ujasusi ya Korea Kusini inaamini kwamba Korea Kaskazini imetuma zaidi ya makombora milioni moja kwa Moscow tangu mwanzo wa Agosti, ikiwa takriban miezi miwili ya utoaji wa silaha kwa Russia kwenye mapigano hayo.

Blinken ameongeza kusema kwamba Russia kwa upande wake inatoa msaada na mafunzo kwenye program za kijeshi za Korea Kaskazini, bila kutoa maelezo zaidi. Wakati wa mkutano wa Septemba kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na rais wa Russia Vladimir Putin mashariki mwa Russia, Putin alionekana kuthibitisha kuwa Moscow inasaidia Pyongyang kutengeneza satellite, ingawa alikubali kuwa vizingiti kadhaa huenda vikahujumu ushirikiano huo.

Forum

XS
SM
MD
LG