Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:17

US, NATO wafuata hatua ya Russia kusitisha mkataba wa Vita Baridi


Bendera za nchi wanachama wa NATO zikiwa nje ya mkutano wa NATO huko Vilnius, Lithuania, Julai 9, 2023.
Bendera za nchi wanachama wa NATO zikiwa nje ya mkutano wa NATO huko Vilnius, Lithuania, Julai 9, 2023.

Washington na washirika wa NATO walisema Jumanne watafuata hatua ya Russia kusitisha mkataba wa Vita Baridi ambao unadhibiti matumizi ya silaha za nyuklia Ulaya, huku White House ikisema ilikuwa “haina chaguo” ila kujitoa. 

Watetezi wanaounga mkono kutosambaa kwa silaha za nyuklia walisema hili halitokuwa na athari kubwa katika uwanja wa vita.

“Kusitisha Mkataba wa majeshi yanayotumia silaha zisizo za nyuklia huko Ulaya (CFE) “utaimarisha uwezo wa ushirika wa [NATO] kuzuia na kujihami kwa kuondoa vikwazo ambavyo vinaathiri mipango, upelekaji majeshi, na mazoezi – vizuizi ambavyo havina uwezo wa kuidhibiti Russia baada ya Moscow kujitoa,” mshauri wa usalama wa taifa Jake Sullivan alisema katika taarifa yake.

Mkataba wa mwaka 1990 ulitengenezwa kuzuia pande zote za muundo wa nguvu za Vita Baridi – katika wakati ambao, Mkataba wa Warsaw kati ya NATO na uliokuwa Umoja wa Soviet – wasiweze kurundika majeshi kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi.

Pia iliweka udhibiti sawa kwa idadi ya vifaru, magari ya kivita, mizinga mizito, ndege za kivita na helikopta za mashambulizi vilivyopelekwa katika eneo hilo lilioko kati ya bahari ya Atlantic na milima ya Ural.

John Kirby, mkurugenzi wa mawasiliano ya kimkakati katika Baraza la Usalama la Taifa, alisema Marekani haikuwa na njia mbadala bora zaidi ila kujiondoa.

“Sidhani vipi tungeweza kuhalalisha kutojitoa katika mkataba huo, ilivyokuwa kwamba Warussia wameamua peke yao kuutupa mkataba huo katika jalala,” alisema.

“Waliiacha Marekani na washirika wetu wa NATO bila ya kitu mbadala ila kusitisha yale tuliyokuwa tunayashikilia na kutekeleza mkataba huo, pia.”

VOA iliuliza iwapo uamuzi huu unaweza kupelekea washirika wa NATO kuongeza uwepo wa silaha zao huko Ukraine.

“Kwa hali ya baadaye, bila shaka sitozungumzia hilo katika jukwaa hili.

NATO ambayo iliikosoa hatua ya Russia kutangaza kujitoa katika mkataba huo mwezi Juni, imejitetea juu ya uamuzi wake kufanya hivyo.

Katika taarifa yao, wanachama 31 wa ushirika huo wa kiulinzi, walisema wote wanaunga mkono kusitisha ushiriki wao “kwa kipindi chochote kile ikiwa ni muhimu kufanya hivyo.”

Ripoti ya Anita Powell, VOA News

Forum

XS
SM
MD
LG