Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 16:45

‘Hidrojeni ya kijani’ kutawala kongamano la biashara la EU-Namibia


Pikipiki ya umeme ikiwa imeegeshwa katika kituo cha kuzalisha hidrojeni ya kijani huko Vredendal, Afrika Kusini Novemba 15, 2022. Picha na REUTERS/Esa Alexander.
Pikipiki ya umeme ikiwa imeegeshwa katika kituo cha kuzalisha hidrojeni ya kijani huko Vredendal, Afrika Kusini Novemba 15, 2022. Picha na REUTERS/Esa Alexander.

Maafisa wa Umoja wa Ulaya na Namibia wanakutana wiki hii katika kongamano la biashara mjini Brussels nchini Ubelgiji kuhusu kuendeleza sekta changa ya "haidrojeni ya kijani" nchini humo.

Wakosoaji wanauelezea mpango huu wa nishati ya kijani kuwa kama aina ya "ukoloni" ambapo Afrika inazalisha zaidi kwa ajili ya Ulaya wakati bara hilo linabaki nyuma kimaendeleo.

Ikionekana kama nishati safi mbadala, hidrojeni ya kijani inatangazwa kuiondoa nishati inayotokana na kaboni kama vile makaa ya mawe na mafuta, ambayo yanalaumiwa kwa ongezeko la joto duniani na uharibifu wa tabaka la ozoni.

Namibia haina miundombinu kwa ajili ya soko la kijani la hidrojeni, lakini imekuwa ikipokea ruzuku kutoka Umoja wa Ulaya, ikiwemo nchi mwanachama Ujerumani, kujenga msingi wa kukidhi mahitaji ya EU ya nishati hiyo.

Mchambuzi wa kisiasa Ndumba Kamwanya amekuwa akitilia shaka msisitizo wa Namibia wa kutaka kuipatia Ulaya hidrojeni ya kijani kibichi na metali muhimu za ardhini, ikiwa ni pamoja na lithiamu, ambayo ni muhimu kwa mpito wa nishati duniani.

Katika mahojiano na VOA, alisema kuwa kusambaza malighafi kwa Ulaya kutaendeleza kile anachokiita ukoloni, ambapo rasilimali zinazotolewa katika bara la Afrika zinatumika katika ukuaji wa viwanda barani Ulaya. Anasema Namibia ina mahitaji yake ya nishati.

Naye Nangula Uauandja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ukuzaji na Maendeleo ya Uwekezaji ya Namibia, inayojulikana kama NIPDB, ambayo inasaidia kuandaa kongamano hilo. Alisema Namibia ina mkakati wa uzalishaji wa ndani na matumizi ya bidhaa za kijani za hidrojeni kama vile maji ya ziada, amonia na brine.

Kongamano la kibiashara la EU-Namibia linafanyika wakati wa Jukwaa la Global Gateway la Umoja wa Ulaya linalofanyika huko Brussels siku ya Jumatano na Alhamisi.

EU ni mshirika mkubwa sana wa kibiashara wa Namibia. Asilimia 26 ya mauzo ya nje ya Namibia yanakwenda EU.

Forum

XS
SM
MD
LG