Makamu Rais Harris amesema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa kimataifa wa kiupanga kanuni na sheria za utumiaji wa teknolojia mpya ya AI.
Mkutano huo unaofanyika kwenye jengo la Bletchley Park, Uingereza unawaleta pamoja viongozi wa kisiasa wa mataifa ya dunia, wafanyabishara, wanasayansi wa teknolojia, na wataalamu wa teknohama kupanga makubaliano ya kwanza ya kimataifa juu ya utumiaji na usalama wa AI ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa raia.
China, Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa kadhaa yamekubaliana Jumatano kwamba watafanya kazi pamoja ili kutayarisha masharti, kanuni na sheria za kulinda utumiaji na teknolojia hiyo ya AI, kwa mkataba utakaofahamika kama “Tangazo la Bletchley.”
Tajiri Elon Musk, mmiliki wa mtandao wa X na makampuni mengine, alieleza wasi wasi mkubwa juu ya maendeleo ya kasi ya program na teknolojia ya AI kwenye mkutano huo wa kwanza wa kilele juu ya usalama wa AI.
Waatalamu wengi wanahofu kwamba mashini na komputa zitakua na akili nyingi zaidi kuliko za binadamu na matokeo yake yatakua athatri ambazo hazijategemewa.
Forum