Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 23, 2024 Local time: 02:31

EU yapitisha vikwazo Niger


Waziri mkuu mteule wa kijeshi wa Niger Minister Ali Mahamane Lamine Zeine
Waziri mkuu mteule wa kijeshi wa Niger Minister Ali Mahamane Lamine Zeine

Nchi wanachama wa umoja wa ulaya jumatatu zimepitisha muundo wa kuwawekea vikwazo maafisa wa utawala wa  kijeshi walionyakua madaraka Niger mwezi julai.

Utaratibu huo mpya utairuhusu EU kuweka vikwazo kwa watu binafsi na taasisi zinazohusika na vitendo vinavyotishia amani , utulivu na usalama wa Niger, kudhoofisha utaratibu wa kikatiba au kujumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu au sheria za kimataifa za kibinadamu , baraza la EU limesema.

Kwa hili, EU inalenga kuangalia na kuimarisha hatua zozote zilizochukuliwa na taasisi wa kikanda ya Afrika Magharibi – ECOWAS.

“ Tangu mwanzo EU imelaani mapinduzi ya Niger kwa maneno makali,”mkuu wa sera za mambo ya nje wa EU Josep Borrell alisema.

“ Kwa uamuzi wa leo , EU inaimarisha uungwaji mkono wake kwa juhudi za ECOWAS , na kutuma ujumbe wa wazi kwamba mapinduzi ya kijeshi yana gharama.

Forum

XS
SM
MD
LG