“Yupo kwenye makao ya Rais mjini Niamey akiwa na mke wake na mtoto wake wa kiume, na ameruhusiwa kupiga simu,” wanafamilia wameongeza. Taarifa zimeongeza kusema kwamba daktari wake aliruhusiwa kumuona, wakati akimpelekea chakula pia.
Utawala wa kijeshi uliomuondoa madarakani Julai 26 Alhamisi ulidai kwamba ulitibua jaribio la kuhepa la Bazoum kutoka alipozuiliwa. Msemaji wa utawala huo alisema kwamba Bazoum alipanga kujificha nje ya Niamey kabla ya kuondoka kwa helikopta ya kigeni, akielekea Nigeria.
Utawala huo umeongeza kusema kwamba baadhi ya wahusika wa mpango huo wamekamatwa. Wakili anayemuwakilisha Bazoum amekanusha madai hayo akisema kwamba ameendelea kuzuiliwa bila mawasiliano.
Forum