Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 22:50

Ukraine yasema kuwa Russia imefanya mashambulizi usiku kucha huko Odesa


Makombora kutoka vikosi vinavyoungwa mkono na Russia yarushwa kuelekea Ukraine. Picha ya maktaba.
Makombora kutoka vikosi vinavyoungwa mkono na Russia yarushwa kuelekea Ukraine. Picha ya maktaba.

Maafisa wa Ukraine wamesema Jumatatu kwamba vikosi vya Russia vimefanya mashambuliziusiku kucha kutumia drone na makombora  wakilenga  maeneo tofauti ya nchi.

Jeshi la anga la Ukraine limesema kwamba limezitungua drone 14 zikiwemo 13 zilizotengenezewa Iran aina ya Shahed, pamoja na kombora. Gavana wa Odesa Oleh Kiper amesema kwamba vifusi kutoka kwenye moja ya drone zilizoangushwa vilianguka upande wa kusini wa mkoa huo na kuharibu ghala kwenye bandari.

Kiper amesema hakuna majeruhi walioripotiwa. Russia imerudia kuilenga Odesa kwa mashambulizi ya anga, pamoja na bandari kwenye Black Sea na mto Danube. Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema kupitia Telegram kwamba mashambulizi ya karibuni ya Russia yamelenga kusini, mashariki na kati kati mwa taifa hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG