Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:04

Afisa wa jeshi la Ukraine anadaiwa kuratibu shambulio katika bomba la Nord Stream

Mfano wa mabomba ya gesi ya asili ya Nord Stream.
Mfano wa mabomba ya gesi ya asili ya Nord Stream.

Hakuna mtu aliyechukua jukumu la milipuko ya Septemba mwaka 2022 kwenye kisiwa cha Bornholm cha Denmark ambayo iliharibu mabomba matatu kati ya manne ya gesi asilia  yanayopita  kwenye Bahari ya Baltic na kupeleka gesi ya Russia hadi Ulaya.

Afisa mmoja wa jeshi la Ukraine anadaiwa kuratibu shambulio la mwaka jana kwenye bomba la gesi asilia la Nord Stream, kulingana na gazeti la Washington Post likinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa nchini Ukraine na Ulaya.

Hakuna mtu aliyechukua jukumu la milipuko ya Septemba mwaka 2022 kwenye kisiwa cha Bornholm cha Denmark ambayo iliharibu mabomba matatu kati ya manne ya gesi asilia yanayopita kwenye Bahari ya Baltic na kupeleka gesi ya Russia hadi Ulaya.

Marekani na NATO, Ushirika wa Mkataba wa Atlantiki Kaskazini-The North Atlantic Treaty Organisation walikiita kitendo hicho kuwa ni hujuma, wakati Moscow ilisema ni kitendo cha ugaidi wa kimataifa.

Ujerumani, Denmark na Sweden zimeanzisha uchunguzi juu ya milipuko ya Nord Stream ilisababisha moshi wa Methane katika anga kufuatia kuvuja kwa siku kadhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG