Mawaziri wa mazingira wa G7 wamejitolea Jumanne kuongeza uzalishaji na kupeleka teknolojia ya kuhifadhi betri sehemu muhimu ya kuongeza nishati mbadala na kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Betri zimekuwa muhimu katika ongezeko la magari ya umeme (EVs) lakini pia ni muhimu kwa nishati ya upepo na jua kwa sababu ya asili ya vyanzo hivi vya nishati. Umeme wa ziada lazima uhifadhiwe katika betri ili kuimarisha usambazaji bila kujali wingi wa mahitaji, au kukatika kwa usambazaji wa huduma wakati wa usiku au wakati upepo unapokuwa mdogo.
Upelekaji wa betri katika sekta ya nishati mwaka jana uliongezeka zaidi ya asilimia 130 kutoka mwaka 2022, kulingana na ripoti iliyotolewa wiki iliyopita na Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA). Masoko makuu ni China, Umoja wa Ulaya na Marekani.
Nchi nyingine znazofuata ni Uingereza, Korea Kusini, Japan na mataifa yanayoendelea barani Afrika, ambako teknolojia ya nishati ya jua na uhifadhi inaonekana kama lango la upatikanaji wa nishati.
Forum