Shirika lisilo la serikali la maendeleo la Uswisi Swissaid lilichapisha ripoti likisema kwamba kati ya tani 321 na 474 za dhahabu kutoka Afrika inayozalishwa kupitia uchimbaji kwa kutumia mikono kwenye migodi midogo inasafirishwa kimagendo kila mwaka, na thamani yake ni kati ya dola bilioni 24 na bilioni 35.
Afrika ni mzalishaji mkubwa wa dhahabu duniani, huku Ghana, Afrika Kusini, Mali na Burkina Faso zikiongoza kwa uzalishaji huo mwaka 2022.
Kulingana na shirika hilo la Uswisi, usafirishaji wa dhahabu ya Afrika kwa njia ya magendo umeongezeka, uliongezeka maradufu kati ya 2012 na 2022.”
Shirika hilo linasema madini hayo ya thamani ni “chanzo cha mapato kwa mamilioni ya wachimbaji wadogo, ni chanzo kikuu cha mapato kwa serikali nyingi, ni bidhaa ya kufadhili makundi yenye silaha, na sababu ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uharibifu wa mazingira.
Ripoti hiyo imeiitaja Dubai kama kitovu cha biashara ya dhahabu ya Afrika, ambayo inasafirishwa kuelekea nchi nyingine ikiwemo Uswisi.
Shirika hilo linakadiria kuwa mwaka 2022, “asilimia 66.5 sawa na tani 405 za dhahabu ilioagizwa kutoka Afrika na kuingizwa ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu ilisafirishwa kimagendo nje ya nchi za Afrika”.
Forum