Wito wa kusitisha mgomo huo ulitolewa na vyama viwili vikuu vya wafanyakazi, the Nigeria Labour Congress (NLC) na Trade Union Congress (TUC), na mgomo umesimamishwa wakati taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika likikabiliwa na mfumko mkubwa wa bei na sarafu ya naira isiyokuwa imara.
Jumatatu, wafanyakazi wa vyama vya wafanyakazi walifunga mtambo wa umeme wa kitaifa, walidumaza safari za ndege za ndani na kufunga ofisi nyingi za serikali, bandari, vituo vya mafuta ya petroli na mahakama ili serikali itosheleze ombi lao la kuongeza kima cha mshahara.
Serikali baadaye Jumatatu ilisema vyama vya wafanyakazi vimekubali wiki nyingine ya mazungumzo ili kujaribu kufikia makubaliano.
Baada ya mashauriano kuhusu msimamo wa serikali na wanachama wao Jumanne, NLC na TUC walisema wameomba mgomo usitishwe kwa siku saba.
Forum