Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:09

Putin asema Russia iko tayari kujenga uhusiano na serikali ya Taliban


Rais wa Russia akuhudhuria mkutano wa wahariri wakuu wa vyombo vya habari vya kimataifa mjini St Petersburg, Juni 5, 2024.
Rais wa Russia akuhudhuria mkutano wa wahariri wakuu wa vyombo vya habari vya kimataifa mjini St Petersburg, Juni 5, 2024.

Rais wa Russia Vladimir Putin Jumatano alitoa wito kwa Moscow “kujenga” uhusiano na serikali ya Taliban, wakati ujumbe wa Taliban ukiitembelea Russia.

“Siku zote tumekuwa tukiamini kwamba tunahitaji kukabiliana na hali halisi. Taliban ambao wako madarakani nchini Afghanistan, tunapaswa kujenga uhusiano na serikali ya Taliban,” Putin alisema katika mkutano na vyombo vya habari vya kigeni.

Putin alikuwa akizungumza kando ya mkutano wa kimataifa wa uchumi wa mjini Saint Petersburg, ambako ujumbe wa Taliban uliwasili Jumatano.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov alisema wiki iliyopita kwamba Moscow inapanga kuwaondoa Taliban kwenye orodha yake ya makundi ya kigaidi yaliyopigwa marufuku karibu miaka mitatu baada ya kundi hilo kunyakua madaraka kutoka kwa serikali iliyokuwa inaungwa mkono na Marekani.

Taliban walitajwa kama kundi la kigaidi nchini Russia tangu mwaka 2003.

Forum

XS
SM
MD
LG