Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 07:54

Guinea Bissau yafunga sehemu ya mpaka wake na Senegal


Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake Afrika Kusini, Aprili 28, 2022. Picha ya AFP
Rais wa Guinea-Bissau Umaro Sissoco Embalo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake Afrika Kusini, Aprili 28, 2022. Picha ya AFP

Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo Jumatano aliliambia shirika la habari la AFP kwamba aliamuru kufungwa kwa sehemu ya mpaka wa nchi yake na Senegal baada ya mapigano makali kuzuka kati ya jamii mbili za Kiislamu.

Jamii hizo mbili kusini mwa Senegal kwa muda mrefu zimekuwa zikizozana juu ya udhibiti wa msikiti mkuu wa eneo hilo na kulaumiana kuwa chanzo cha mivutano iliyosababisha vifo vya watu kadhaa hapo awali.

Wakati wa siku kuu ya Eid Jumatatu, mapigano kati ya jamii hizo yalizuka katika mji mtakatifu wa Medina Gounass, umbali wa kilomita chache kutoka Guinea-Bissau.

Mtu mmoja aliuawa na wengine 20 kujeruhiwa kulingana na wizara ya mambo ya ndani.

Rais Embalo alisema kufuatia mapigano ya Jumatatu, “moja ya jamii inayoishi Guinea-Bissau ilitoa wito wa kuimarisha usalama.”

“Mara moja nilichukua uamuzi wa kufunga sehemu hiyo ya mpaka ili kuzuia ongezeko lolote la ghasia. Vyombo vya usalama vya nchi yangu vinahakikisha kwamba hatua hii inaheshimiwa kwa uangalifu mkubwa,” aliongeza.

Senegal na Guinea Bissau zina mpaka wa kilomita 300.

Forum

XS
SM
MD
LG