Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 04, 2024 Local time: 08:35

Watu 39 wameuawa katika maandamano nchini Kenya :Tume ya haki za binadamu


Polisi wakikabiliana na waandamanaji mjini Nairobi, Kenya, Juni 25, 2024.
Polisi wakikabiliana na waandamanaji mjini Nairobi, Kenya, Juni 25, 2024.

Jumla ya watu 39 waliuawa katika maandamano dhidi ya serikali nchini Kenya, tume ya kitaifa ya haki za binadamu ilisema Jumatatu, huku wanaharakati wakiongeza juhudi za kuitisha duru nyingine ya maandamano wiki hii.

Idadi hiyo ni maradufu ya ile iliyotolewa awali na mamkala kuhusu watu waliouawa wakati wakiandamana kupinga nyongeza ya ushuru.

“Takwimu kutoka kwa rekodi zetu zinaonyesha kuwa watu 39 wamekufa na 361 kujeruhiwa kuhusiana na maandamano ya nchi nzima,” tume hiyo ya haki za binadamu inayofadhiliwa na serikali ilisema katika taarifa, na kuongeza kuwa takwimu hizo zinahusu kipindi cha kuanzia Juni 18 hadi Julai 1.

Ilisema pia kuwa kuna kesi 32 “za watu waliotoweka” na waandamanaji 627 waliokamatwa.

Maandamano hayo yakiongozwa hasa na vijana, yalifanyika kwa amani kwa kiasi kikubwa, lakini yaligeuka kuwa vurugu mbaya Jumanne wakati wabunge walipopitisha mswaada wa fedha wenye utata.

Baada ya mswaada huo kupigiwa kura, umati wa watu ulishambulia jengo la bunge mjini kati Nairobi na sehemu ya jengo hilo kuchomwa huku polisi wakiwafyatulia risasi waandamanaji.

Rais William Ruto alisema katika mahojiano na televisheni Jumapili kwamba watu 19 walifariki katika maandamano, na kusisitiza kuwa “ hahusiki kamwe katika umwagaji damu” na kauhidi uchunguzi kuhusu vifo hivyo.

Forum

XS
SM
MD
LG