ANC, ambacho kimeiongoza nchi tangu ujio wa demokrasia mwaka 1994, kimepata wizara 20 kati ya 32, zikiwemo wizara ya mambo ya nje, fedha, ulinzi, sheria na polisi.
Mshirika mkuu, the Democratic Alliance (DA), kitakuwa na wizara sita zikiwemo mambo ya ndani, mazingira na ujenzi.
Kiongozi wa DA John Steenhuisen, ameteuliwa kuwa waziri wa kilimo.
Chama cha Wazulu cha Inkhata Freedom (IFP) na vyama vingine vidogo vilipata jumla ya wizara 6, zikiwemo wizara ya mageuzi ya ardhi, huduma ya magereza, michezo, utalii na utumishi wa umma.
“Uundwaji wa serikali ya Umoja wa kitaifa katika hali yake ya sasa ni mfano ambao hujawahi kushuhudiwa katika historia ya demokrasia yetu, Ramaphosa alisema, akizungumza kutoka mjini Pretoria katika hotuba kwa njia ya televisheni.
Alichaguliwa kwa muhula wa pili wiki iliyopita, kuongoza kile chama chake kimetaja kuwa serikali ya Umoja wa kitaifa baada ya ANC kupoteza wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Mei.
“Serikali inayokuja italipa kipaumbele suala la ukuaji wa uchumi wa haraka, shirikishi na endelevu na kuunda jamii yenye uadilifu zaidi ili kukabiliana na umaskini na ukosefu wa usawa pamoja na ukosefu wa ajira,” alisema.
Forum