Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 10:47

Ruto asema hawezi kulaumiwa kwa mauaji yaliyotokea katika maandamano


Rais William Ruto akilihutubia taifa kwenye Ikulu, Juni 26, 2024. Picha ya AP
Rais William Ruto akilihutubia taifa kwenye Ikulu, Juni 26, 2024. Picha ya AP

Mamia ya watu waliandamana Jumapili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, kuwaenzi wale waliofariki katika maandamano ya kuipinga serikali wiki iliyopita, huku Rais William Ruto akisisitiza kwamba, na hapa ninamnukuu: “Sihusiki katika umwagaji damu.”

Makundi ya haki za binadamu yanasema watu 30 walifariki katika maandamano yaliyochochewa na hatua ya serikali ya kuongeza ushuru katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kufuatia ghasia hizo, Ruto alitangaza kubadili msimamo mapema wiki iliyopita, akisema “atawasikiliza wananchi” na hatasaini mswaada wa fedha kuwa sheria.

Katika mahojiano na televisheni, Ruto alisema watu 19 walikufa, ikiwa idadi ya kwanza kutolewa na mamlaka na kuahidi uchunguzi kamili kuhusu vifo hivyo.

Maandamano ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani yaligeuka kuwa ya vurugu Jumanne iliyopita wakati wabunge walipopitisha nyongeza ya ushuru inayopingwa na wengi kufuatia shinikizo kutoka shirika la kimataifa la fedha (IMF).

Polisi walifyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge na moto ukazuka.

“Sijahusika katika umwagaji damu,” Ruto alisema katika mahojiano na televisheni ya Kenya.

Akizungumzia vifo hivyo, alisema “ Ni hali ya kusikitisha sana. Kama taifa la kidemokrasia, hali kama hiyo haikutakiwa kugubika mjadala wetu.”

Aliongeza kuwa “Uchunguzi utafanyika kuhusu jinsi watu hao 19 walivyofariki.”

“Maelezo yatatolewa kuhusu kila kifo.”

Ruto alisema “Polisi walijarubu kufanya wawezavyo.”

“Iwapo kumekuwa na kutumia nguvu kupita kiasi, tuna njia za kuhakikisha kwamba utumiaji huo wa nguvu kupita kiasi unashughulikiwa.”

Forum

XS
SM
MD
LG