Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 19:23

Rais wa Nigeria atenga dola bilioni 1.3 kukabiliana na mfumko wa bei


Rais wa Nigeria Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Tinubu

Rais wa Nigeria amependekeza kitita cha dola bilioni 1.3 kukabiliana na kupanda kwa bei na ukosefu wa usalama wa chakula huku nchi hiyo ikipambana na mzozo mbaya wa kiuchumi, waziri wa fedha alisema Alhamisi.

Kitita hicho cha naira trilioni mbili bado tu ni mpango huku Bola Ahmed Tinubu akikabiliwa na shinikizo kupunguza mzigo wa mageuzi ya kiuchumi aliyoleta baada ya kuwa rais mwaka jana.

Tinubu aliondoa ruzuku ya mafuta na udhibiti wa sarafu ya nchi, hali ambayo ilisababisha bei ya petroli kupanda mara tatu na kupanda kwa gharama ya maisha, huku thamani ya naira ikishuka dhidi ya dola ya Marekani.

Hatua hizo ziliwaumiza sana wananchi na Wanigeria wengi wamelazimika kuacha kupata baadhi ya milo, huku mzozo wa kiuchumi kaskazini mwa nchi ukiwalazimisha watu kula mchele wa kiwango duni unaotumiwa sana kama chakula cha samaki.

Waziri wa fedha Wale Edun aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza jipya lililoundwa na rais kusaidia “kuweka pamoja uwezo wa kifedha kwa kuzingatia kitita hicho cha naira trilioni 2.”

Eden alisema kitita hicho kinajumuisha dola milioni 229 kwenye sekta ya afya na ustawi wa jamii na karibu dola milioni 328 kwa ajili ya kilimo na usalama wa chakula.

“Kipaumbele cha kwanza cha Rais ni kuhusu uzalishaji wa chakula, usalama wa chakula na usalama wa lishe,” Edun alisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG