Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 10:57

Viongozi wa Chadema waachiliwa kwa dhamana, chama kinadai walipigwa


Viongozi wa chadema na wafuasi wa chama wakiandamana jijini Dar Es Salaam, Januari 24, 2024. Picha ya AP
Viongozi wa chadema na wafuasi wa chama wakiandamana jijini Dar Es Salaam, Januari 24, 2024. Picha ya AP

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema Jumanne kilidai kwamba viongozi wake kadhaa walipigwa wakati wa kamata kamata ya watu wengi kabla ya mkutano uliopigwa marufuku.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na naibu wake Tundu Lissu na maafisa wengine wakuu waliachiliwa kwa dhamana Jumanne kufuatia kukamatwa kwao kabla ya mkutano wa vijana wanachama ulikuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumatatu katika mji wa kusini magharibi wa Mbeya.

Naibu katibu mkuu wa chama Benson Kigaila alisema, Lissu pamoja na katibu mkuu wa chama John Mnyika na mkuu wa chama katika eneo la kusini la Nyasa Joseph Mbilinyi “walipigwa vibaya” wakati wa kukamatwa kwao.”

Kigaila alisema viongozi waliokuwa wameshikiliwa walisafirishwa kutoka Mbeya hadi Dar Es Salaam ambako waliachiliwa Jumanne.

“Baada ya kuachiliwa kwao Jumanne asubuhi, walikwenda wenyewe hospitali na tutawahamisha hali yao ya afya baadaye,” aliongeza.

Awadh Haji, mkuu wa polisi anayehusika na operesheni na mafunzo alithibitisha kuachiliwa kwa viongozi wa Chadema lakini akaonya kwamba polisi watachukua “hatua kali dhidi ya mtu yeyote au kundi litakalohusika katika kuvuruga amani”.

Forum

XS
SM
MD
LG