Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:32

DRC yasikitishwa na kitendo cha maafisa wa polisi kuwashambulia wanadiplomasia wa Ufaransa


Rais wa DRC Tshisekedi akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris, Aprili 30, 2024. Picha ya Reuters
Rais wa DRC Tshisekedi akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris, Aprili 30, 2024. Picha ya Reuters

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu ilielezea masikitiko yake juu ya kitendo cha kushambuliwa kwa wanadiplomasia watatu wa Ufaransa katika mji mkuu Kinshasa, vyanzo vya serikali na kidiplomasia viliiambia AFP.

Maafisa wa polisi ni miongoni mwa kundi lililovamia jengo linalotumiwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa lengo la “kumfukuza mwanadiplomasia wa Ufaransa”, wizara ya sheria ilisema katika taarifa.

Mwanadiplomasia anayehusika na ushirikiano wa kitamaduni kwenye Ubalozi alipigwa alipokuwa akishikiliwa kwa karibu saa tatu, huku wanadiplomasia wengine wawili wakisukumwa bila kupata majeraha”, chanzo cha kidiplomasia kiliongeza.

Wizara ya sheria ilisema “ Maafisa wa polisi na mfanyakazi wa ofisi ya mwendesha mashtaka ni miongoni mwa washambuliaji, na baadhi yao walikamatwa.”

Balozi wa Ufaransa Bruno Aubert alikutana na Rais Tshisekedi Jumatatu.

Waziri wa mambo ya nje wa DRC Therese Wagner Kayikwamba tayari alielezea masikitiko yake makubwa Jumamosi juu ya tukio hilo ambalo limekiuka mikataba ya kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG