Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 12:21

Shambulizi la kombora la Russia kwenye bandari ya Ukraine laua watu sita


Picha hii inaonyesha kituo cha nafaka katika bandari ya Ukraine ya Odesa, katika Bahari ya Black Sea. Picha ya Reuters
Picha hii inaonyesha kituo cha nafaka katika bandari ya Ukraine ya Odesa, katika Bahari ya Black Sea. Picha ya Reuters

Kombora la masafa marefu la Russia kwenye bandari katika mkoa wa kusini mwa Ukraine wa Odesa liliua watu sita na kujeruhi wengine 11 Jumatano, maafisa walisema.

Shambulizi hilo lililenga meli ya mizigo ya kiraia yenye bendera ya Panama, kulingana na gavana wa Odesa Oleg Kiper.

“Watu sita waliuawa, wote ni raia wa Ukraine,” Kiper alisema kwenye mtandao wa Telegram.

Alisema baadaye kwamba idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka hadi watu 11.

“Hili ni shambulizi la tatu kwenye meli ya kiraia katika siku nne zilizopita,” gavana huyo aliongeza.

Russia ililenga mkoa huo wa pwani wa Ukraine katika vita vyake, ikishambulia boti na meli za nafaka katika kile Kyiv inasema ni jaribio haramu la kuharibu uwezo wake wa kuuza nje bidhaa zake.

Ukraine ilikuwa mmoja ya wauzaji wakubwa wa nafaka duniani kabla ya uvamizi wa Russia mwezi Februari mwaka 2022, lakini mashambulizi ya mara kwa mara kwenye bandari yake na kwenye maghala yake yamepunguza sana pato lake.

Forum

XS
SM
MD
LG