Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 15, 2024 Local time: 06:25

Waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini wamuondolea mashtaka Rais Ramaphosa


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Mamlaka ya kuendesha mashtaka nchini Afrika Kusini Alhamisi ilisema haitaendelea na mashtaka ya utakatishaji fedha na ufisadi dhidi ya Rais Cyril Ramaphosa yanayohusiana na wizi wa dola za Marekani uliofanyika kwenye shamba lake mwaka 2020.

Mkuu wa zamani wa kitengo cha ujasusi aliwasilisha malalamiko ya jinai dhidi ya Ramaphosa kufuatia wizi katika shamba lake la la Phala Phala kaskazini mashariki mwa jimbo la Limpopo, akidai kuwa rais alifanya makosa kwa kujaribu kuficha wizi wa dola milioni 4 taslimu.

Kufuatia uchunguzi wa kitengo maalum cha polisi, mwendesha mashataka wa Limpopo “amechukua uamuzi wa kutomshtaki mtu yeyote”, mamlaka ilisema katika taarifa.

“Amebaini kuwa hakuna matarajio ya msingi ya kufungua mashtaka kulingana na ushahidi uliomo katika kesi hiyo.”

Mamalamiko hayo yalidai Ramaphosa alihusika katika utakatishaji wa fedha na ufisadi kuhusiana na wizi huo, taarifa hiyo ilisema.

Forum

XS
SM
MD
LG