Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 17:07

Makamu wa Rais wa Kenya akanusha tuhuma za ufisadi dhidi yake


Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua
Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua Jumatatu alikanusha madai ya ufisadi dhidi yake katika mkesha wa kura ya kutokuwa na Imani naye ambayo inaashiria mgawanyiko mkubwa katika chama tawala.

Tuhuma hizo “zinakasirisha” na ni “propaganda tupu”, Gachagua alisema katika mkutano na waandishi wa habari, akizitaja kuwa jaribio la “kuniondoa madarakani kutokana na sababu nyingine za kisiasa”.

Hakuna mashtaka rasmi yaliyofunguliwa na waendesha mashtaka na hakuna uchunguzi ulionzishwa na mahakama.

Lakini Gachagua alishindwa kuzuia mchakato wa kutokuwa na na imani naye katika bunge wiki iliyopita, licha ya kuwasilisha malalamiko mara kadhaa mahakamani akiomba mchakato huo usitishwe.

Makamu huyo wa Rais William Ruto anatuhumiwa ufisadi, kudhoofisha shughuli za serikali na kutumia siasa za kikabila zinazoleta mgawanyiko, kati ya mashtaka mengine.

Wabunge wa Kenya walianzisha mchakato wa kumfungulia mashtaka tarehe 1 Oktoba, huku wabunge 291 wakiunga mkono hoja hiyo, ikiwa zaidi ya kiwango cha wabunge 117 kinachohitajika.

Forum

XS
SM
MD
LG