Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 16:57

Mgombea wa upinzani Namibia apinga matokeo ya uchaguzi wa rais


Panduleni Itula, mgombea kiti cha rais wa chama cha upinzani cha Independent Patriots for Change (IPC), cha Namibia akizungumza na waandishi habari mjini Windhoek on November 29, 2024.
Panduleni Itula, mgombea kiti cha rais wa chama cha upinzani cha Independent Patriots for Change (IPC), cha Namibia akizungumza na waandishi habari mjini Windhoek on November 29, 2024.

Mgombea wa chama kikuu cha upinzani nchini Namibia, Panduleni Itula, Jumamosi alisema kwamba chama chake hakitatambua matokeo ya uchaguzi wa rais wenye utata uliogubikwa na vurugu na madai ya wizi wa kura.

Akizungumza muda mfupi kabla ya vituo vya kupigia kura kufungwa katika siku ya mwisho ya upigaji kura, Itula, ambaye chama chake cha Independent Patriots for Change (IPC) kilikuwa na matumaini ya kuumaliza utawala wa miaka 34 wa chama cha SWAPO, alisema bila kujali matokeo,” IPC hakitatambua matokeo ya uchaguzi huo”.

“Utawala wa sheria umekiukwa kwa kiasi kikubwa na hatuwezi kusema kwa njia yoyote au kipimo chochote kwamba uchaguzi huu ulikuwa huru, wa haki na halali,” alisema Itula, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa 2019.

Huku asilimia chache ya kura zikiwa zimehesabiwa katika maeneo bunge 10 tu kati ya 121 ya nchi hiyo, matokeo ya awali yalionyesha mgombea wa chama cha SWAPO, Makamu wa rais Netumbo Nandi, akiongoza kwa asilimia 48 ya kura akifuatiwa na Itula kwa asilimia 29.

Forum

XS
SM
MD
LG