Wapatanishi kutoka karibu nchi 200 wanakutana kwa faragha kujadili mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa plastiki. Ikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya wapatanishi kukubaliana juu ya mpango wa kwanza wa dunia wa kushughulikia taka za plastiki , rasimu mpya iliyotolewa leo ijumaa imeonyesha kuna kutokukubaliana kwa kiwango cha juu.
Lengo la waliohudhuria ni kuandaa makubaliano kufikia Jumapili, na kuhitimisha miaka miwili ya mazungumzo juu ya makubaliano ya kihistoria.
Saa 48 tu kabla ya mazungumzo yaliyopangwa kukamilika, makubaliano ya awali yaliyotolewa na mwanadiplomasia aliyekuwa mwenyekiti wa mchakato huo yaliibuka, yakiwa na maono yanayoshindana na kutokuelewana.
Kuna ufafanuzi nane uliotolewa kukabili plastiki pekee lna maono tano ya jinsi ya kukabili tishio la plastiki.
Forum