Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 06:55

Wanaharakati wa mazingira wameandamana Nairobi kuzuia uzalishaji wa Plastiki

Mfano wa Plastiki ambazo zinatumika kutengenezea vifaa mbali mbali
Mfano wa Plastiki ambazo zinatumika kutengenezea vifaa mbali mbali

Wawakilishi kutoka zaidi ya mataifa 170 watakutana jijini Nairobi Jumatatu kujadili hatua madhubuti zinazopaswa kujumuishwa katika mkataba wa kimataifa wa kukomesha uchafuzi wa plastiki.

Mamia ya wanaharakati wa mazingira waliandamana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi leo Jumamosi wakitaka hatua kali zichukuliwe kuzuia uzalishaji wa plastiki kabla ya mkutano wa kujadili mkataba wa kimataifa wa plastiki.

Wawakilishi kutoka zaidi ya mataifa 170 watakutana jijini Nairobi Jumatatu kujadili hatua madhubuti zinazopaswa kujumuishwa katika mkataba wa kimataifa wa kukomesha uchafuzi wa plastiki.

Waandamanaji walibeba mabango yenye ujumbe “Mgogoro wa Plastic, ni mgogoro wa hali ya hewa” na “komesha kusambaa kwa sumu katika vizazi vingi”. Walipiga kelele “waache wachafuzi walipe gharama” walipokuwa wakitembea polepole nyuma ya bendi wakitokea katikati ya Nairobi kuelekea eneo la bustani, magharibi mwa mji mkuu.

Mataifa yalikubaliana mwaka jana kukamilisha mkataba wa kwanza wa Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka 2024 wa kushughulikia janga la plastiki, lililopo kila mahali kuanzia kwenye vilele vya mlima hadi ndani ya bahari, na ndani ya damu ya binadamu pamoja na maziwa ya mama.

Forum

XS
SM
MD
LG