Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:41

Dunia yatakiwa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa


Watu waliojitolea wakiwa wamebeba mifuko iliyojaa uchafu wa plastiki katika kaunti ya Kilifi, Kenya. Picha na Simon MAINA / AFP.
Watu waliojitolea wakiwa wamebeba mifuko iliyojaa uchafu wa plastiki katika kaunti ya Kilifi, Kenya. Picha na Simon MAINA / AFP.

Wapatanishi wa masuala ya mazingira watakutana Ottawa, Canada Jumanne kwa duru ya nne ya mazungumzo kuhusu kile ambacho kitakuwa mkataba wa kwanza wa kimataifa juu ya kuongezeka kwa uchafuzi wa plastiki.

Mkataba unatolewa wa plastiki umeelezewa kuwa unaweza kuwa mpango muhimu zaidi wa mazingira tangu makubaliano ya hali ya hewa ya Paris ya 2015 lakini wana mazingira wana kibarua kigumu Ottawa, na pande zinazohusika zikiwa mbali sana na hatua ya makubaliano.

Umoja wa Ulaya na mataifa kadhaa, ikiwa ni pamoja na Japan, Canada, na Kenya wametoa wito wa kuwepo kwa mkataba madhubuti wenye "vifungu vya kisheria" kwa ajili ya kupunguza uzalishaji na matumizi ya plastiki zinazotokana na kemikali za petroli na kuondoa au kuzuia plastiki yenye matatizo, kama vile PVC .

Wakati huo huo, mamilioni ya watu duniani wanaadhimisha siku ya Mazingira Duniani kwa shughuli tofauti za kusafisha mazingira yao na kuchukua hatua ya kupunguza matumizi ya plastiki.

Kauli mbiu ya mwaka huu 'Sayari dhidi ya Plastiki'. Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) lilianzisha siku hii mwaka wa 2009, na iliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2010.

UNGA ilitangaza siku hii ili kutambua ukweli kwamba dunia na mazingira yake ni makazi ya kawaida ya binadamu na tunahitajika kuilinda dunia ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuimarisha maisha ya watu, na kukomesha kuporomoka kwa viumbe hai.

Siku ya Mazingira Duniani hutumika kama mwito wa kuchukua hatua kwa watu binafsi, serikali, wafanyabiashara na mashirika ya kiraia kufanya kazi pamoja kuelekea ulimwengu wa kijani kibichi na endelevu zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG