Hatua hii ni mwisho wa kampeni ya muda mrefu ya kisheria dhidi ya kutochukua hatua kwa serikali ya Uswizi katika kupunguza gesi chafu inayosababisha mabadiliko ya tabia nchi.
Anne Mahrer, rais mwenza wa KlimaSeniorinnen, kikundi cha wanawake wazee wa Uswizi 2000 amesema uamuzi wa leo ni uamuzi wa kihistoria," huku akiongeza kuwa joto linalotokana na mabadiliko ya hali ya hewa liliwaweka kwenye hatari za kiafya au vifo vya mapema.
Mwakilishi kutoka serikali ya Uswizi alisema itachukua muda kwa serikali ya Uswizi kutafuta njia sahihi ya kushughulikia uamuzi wa mahakama kwamba kutochukua hatua kwa serikali juu ya mabadiliko ya hali ya hewa kumekiuka baadhi ya haki za binadamu, na akabainisha kuwa mahakama nyingine za kitaifa zina uwezekano wa kuangalia matokeo ya hukumu ya leo.
Mahakama ilitupilia mbali kesi mbili kama hizo leo Jumanne, ya kwanza iliyoletwa na vijana wa Ureno dhidi ya serikali 32 za Ulaya na nyingine na meya wa zamani wa Ufaransa dhidi ya serikali ya Ufaransa.
Forum