Maafisa wawili wa polisi walimnyanyua Thunberg na kumburuza umbali wa mita 20 kutoka katika mlango aliokuwa anawazuia watu wasiingie kabla ya kumlaza chini.
Polisi wa Stockholm walisema kuwa licha ya wanaharakati hao kuwa na haki ya kukusanyika nje ya bunge, kati ya watu watano na 10 waliondolewa kwa sababu ya kuziba mlango wa kuingilia. Walikataa kutoa maelezo kuhusu watu waliokamatwa.
Thunberg na darzeni ya wanakampeni wengine wa mazingira walianza kuzuia lango kuu la kuingia katika bunge la Sweden Jumatatu katika mgomo wa kuinga dhidi ya athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kile walichosema ni uksoefu wa hatua za kisiasa.
Wanaharakati hao waliondoka Jumatatu mchana na kurejea kuendelea na mgomo wao Jumanne asubuhi.
Thunberg, 21, amekuwa kioo cha wanaharakati vijana wa hali ya hewa kutokana na maandamano ya kila wiki aliyokuwa anafanya, kuanzia mwaka 2018, mbele ya bunge la Sweden ambayo haraka yalikuwa ni harakati za vijana kimataifa huku kukiwa na mikutano kadhaa katika mabara yote ulimwenguni.
Mwaka jana Thunberg alikamatwa na polisi au kuondolewa kutoka katika maandamano katika nchi kadhaa ikiwemo Sweden, Norway na Ujerumani.
Mahakama moja Uingereza mwezi uliopita ilimfutia mashtaka yaliyomkabili ya kuvunja utulivu wa umma huku jaji akitoa hukumu kwamba polisi walikuwa hawana mamlaka ya kumkamata yeye na wengine katika maandamano yaliyofanyika Uingereza mwaka jana.
Forum