Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:35

Viongozi wa dunia kuhutubia Mkutano wa UN


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifungua kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA. New York, Marekani, Septemba 24, 2019. REUTERS/Lucas Jackson
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifungua kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA. New York, Marekani, Septemba 24, 2019. REUTERS/Lucas Jackson

Viongozi wa dunia ambao wanashiriki katika masuala muhimu ya siasa za kikanda zenye umaarufu zaidi ni kati ya wale waliopangiwa kuzungumza siku ya kwanza (Jumanne) ya Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York.

Baada ya hotuba ya ufunguzi ya Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, wale waliokusanyika katika mkutano huu wa kila mwaka watapata taarifa kutoka katika kikundi watakacho kuwemo Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Korea Moon Jae-in na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Hotuba hizo mbalimbali zinakuja siku moja baada ya mwanaharakati kijana raia wa Sweden Greta Thunberg alipopaza sauti kuwataka viongozi wa dunia wanaohudhuria kilele cha mkutano wa UN kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, akisema watu wanaathirika na kufa kutokana na kuongezeka kwa joto duniani na kuwa viongozi wote wamekuwa wanatoa matamko matupu bila ya kuchukuwa hatua yoyote.

“Tuko mwanzo wa kuangamia kwa wanadamu na kile pekee mnachozungumzia ni fedha,” amesema Thunberg, ambaye alianzisha harakati za vijana kwa kule kususia kwake masomo siku ya Ijumaa akitaka hatua zichukuliwe dhidi ya uharibifu wa mazingira.

Msichana huyo amesema sayansi imekuwa ikiweka wazi kwa miaka 30, lakini bado viongozi hawajachukuwa hatua za kutosha.

“Viongozi mnatuangusha! Lakini vijana tayari wameanza kuelewa usaliti wenu,” Thunberg amesema katika sauti iliyokuwa imejaa hisia.” Macho ya vizazi vyote vijavyo yanawaangalia nyie. Na kama mkichagua kutuangusha, nawambia hatutawasamehe kamwe.”

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 16 aliwaonya marais zaidi ya 60 na mawaziri wakuu waliokusanyika katika ukumbi wa Baraza Kuu kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo na kuwa vijana hawatawaacha “wasiwajibishwe kwa suala hili.” Amesema wanapiga mstari hapa na hivi sasa "mabadiliko yanakuja" wapende au wasipende.

“Kizazi changu kimefeli kutekeleza majukumu yake kulinda dunia yetu,” Guterres amesema. “Hili lazima libadilike.”

Guterres ametaka kuwepo utaratibu wa kuondoa uzalishaji wa makaa yam awe na kusimamisha kabisa ujenzi wa viwanda vipya vya kuzalisha umeme unaotokana na makaa ya mawe.

“Hivi kweli ni busara kuendelea kujenga viwanda vya makaa yam awe ambavyo vinaangamiza mustakbali wetu?” katibu mkuu amehoji. “Je ni busara kuendelea kutoa motisha kwa uchafuzi wa hali ya hewa ambao unauwa mamilioni ya watu na hewa chafu na kuhatarisha maisha ya watu mijini duniani kote kiasi cha watu hao kuhama makazi yao.

XS
SM
MD
LG