Mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi wa Pakistan nchini Kenya yalikuwa “mauaji yaliyopangwa” timu ya wachunguzi wa Pakistani imesema katika ripoti iliyotolewa Jumatano.
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, lilifanikiwa tena kuwafukuza waasi wa M23 na katika maeneo kadhaa ya wilaya ya Rutshuru.
Rais Samia pia ameihakikishia dunia kuwa chini ya usimamizi wake, Tanzania itaendelea kuwa mwanachama hai wa UN, mshirika wa kutegemewa katika ushirikiano wa kimataifa na “tutaendelea kukunjua mikono yetu kwa wote watakaotaka kutupokea na kushirikiana nasi.”
Juhudi za kidiplomasia za kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza zinaendelea Jumatano.
Mlipuko wa Volcano kwenye mlima Nyiragongo mjini Goma umesababisha maelfu ya watu kutoka Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kukimbilia Rwanda Jumamosi na baada ya hali kuwa shwari siku ya Jumatatu, wakazi waelezea athari za volcano.
Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Jenerali Constant Ndima amesema wakati hayo yakijiri mjini Goma, matope ya moto yamekuwa yakiteremka katika mlima Nyiragongo na kuishia nje kidogo ya mji wa Goma.
Mapambano mapya yamezuka Jumatatu kati ya vikosi vya usalama vya Israeli na Wapalestina waliokuwa wanafanya ibada karibu na msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem Jumatatu.
Taarifa iliyotolewa Jumapili na mwanadiplomasia mwandamizi wa Korea Kaskazini, ilikuwa ni jibu la kwanza rasmi la nchi hiyo baada ya kuijadili sera ya uongozi wa Biden iliyokamilishwa hivi karibuni, inayoeleza uwazi wa kufanya mazungumzo na nchi hiyo yenye kujihami kwa silaha za nyuklia.
Watoto ambao wanakimbia vita na umaskini hutumia usafiri hatari wa baharini kuelekea Ulaya, ulijumuisha watoto 114 waliosafiri peke yao, UNICEF imeongeza katika taarifa yake.
Mkuu wa huduma za sera za mambo ya nje katika EU Josep Borrell amesema katika taarifa yake kuwa wajumbe kutoka Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Iran na Russia watakutana ana kwa ana majira ya saa tisa mchana (1300 GMT).
Rais wa Marekani Joe Biden akihutubia mbele ya bunge Jumatano usiku tangu achukuwe hatamu za uongozi, na kuainisha mpango wake wa dola trillioni 4.
Wanamgambo wa Palestina katika Ukingo wa Gaza wamerusha takriban roketi darzeni tatu ndani ya eneo la Israeli usiku wa kuamkia Jumamosi, wakati jeshi la Israeli likijibu mashambulizi kulenga sehemu zinazo simamiwa na kikundi cha Hamas.
Baada ya miaka 4 ya suala hilo kupuuziwa na Marekani chini ya uwongozi wa rais wa zamani Donald Trump, mkutano huo wa kilele utakuwa “ni fursa kwa Marekani kurejea uwanjani kuonyesha inachukulia suala la mazingira kwa umakini mkubwa,”...
Maelfu wameukimbia mji huo wenye wakazi 75,000 ambapo darzeni ya raia waliuawa, kulingana na idadi iliyotolewa na serikali hapo awali, na kampuni kubwa ya nishati ya Total imeondoka katika eneo ambapo mradi wa gasi uliogharimu mabilioni ya dola unaendelezwa.
Matamshi ya "mstari mwekundu" hauvukwi yametolewa na Spika wa Baraza la Seneti la Jordan, Faisal al-Fayez siku moja tu baada ya maafisa kadhaa waandamizi kukamatwa pamoja na kaka wa kambo wa Mfalme Abdulla wa pili, ambaye amewekwa kizuizini nyumbani.
Polisi huko Bungeni wamesema mshukiwa huyo alitoka kwenye gari akiwa na kisu mkononi na kuelekea kuwashambulia maafisa wa polisi. Polisi hao walimfyatulia risasi. Mshukiwa huyo ametajwa kuwa ni Noah Green, ana umri wa miaka 25.
Darzeni wameuawa na zaidi wa watu 8,000 wamelazimika kukimbia makazi yao na wengi bado hawajulikani walipo kufuatia mashambulio yaliyopangwa na kuwa ni ongezeko la kiwango cha juu la uasi wa kikundi cha Kiislam uliolikumba Jimbo la Cabo Delgado tangu mwaka 2017.
Muda wa kutotoka nje usiku nchi nzima umerekebishwa kwa maeneo husika ikiwemo Kaunti za Nairobi, Kiambu, Kajiado na Nakuru, na sasa amri hiyo itaanza kutekelezwa saa mbili usiku hadi saa kumi Alfajiri.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi wa Mataifa ya Nchi mbalimbali Duniani na Wananchi wa Jiji la Dodoma kwenye Mazishi ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa hayati Rais John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma leo March 22,2021.
Wajane, wakiwa na watoto, wanaishi katika ghala iliyotolewa msaada – zaidi ya watu 180 wamepewa vyumba vilivyo tenganishwa kwa vitambaa au plastiki. Wanawake mara nyingi wanakaa pamoja katika kituo hicho, wakizungumza huku wakichambua mahindi ili kutengeneza chakula cha asili kinachoitwa bisko.
Pandisha zaidi