Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:13

Mvutano Jerusalem wazusha mashambulizi kati ya Hamas na Israeli


 Israel Map State
Israel Map State

Wanamgambo wa Palestina katika Ukingo wa Gaza wamerusha takriban roketi darzeni tatu ndani ya eneo la Israeli usiku wa kuamkia Jumamosi, wakati jeshi la Israeli likijibu mashambulizi kulenga sehemu zinazo simamiwa na kikundi cha Hamas.

Mfululizo wa roketi zilifyatuliwa wakati mamia ya Wapalestina wakipambana na polisi wa Israeli mashariki ya Jerusalem.

Mapambano hayo, ambapo polisi wasiopungua wanne na waandamanaji sita walijeruhiwa, yamekuwa ni matukio ya kila usiku katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan na hakuna dalili ya kusitishwa.

Mzee wa Kipalestina akisoma Quran katika msikiti wa Nuseirat ulioko katika kambi ya wakimbizi, katikati ya Ukingo wa Gaza, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Aprili 18, 2021. (Photo by MAHMUD HAMS / AFP)
Mzee wa Kipalestina akisoma Quran katika msikiti wa Nuseirat ulioko katika kambi ya wakimbizi, katikati ya Ukingo wa Gaza, wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Aprili 18, 2021. (Photo by MAHMUD HAMS / AFP)

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, Tor Wennesland, amelaani ghasia hizo na kusema UN inashirikiana na pande zote husika kurejesha utulivu.

“Vitendo vya uchokozi kuelekea Jerusalem lazima vikome. Kufyatuliwa ovyo kwa roketi kuelekea upande wa maeneo ya makazi ya Waisraeli inakiuka sheria za kimataifa na lazima kusitishwa mara moja,” amesema.

“Nasisitiza wito wangu kwa pande zote kujizuia kadiri wanavyoweza na kuzuia kuongezeka mgogoro huu, hususan wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan na hali tete ya kisiasa kwa wote.”

Wapalestina wakiandaa eneo la kufanya ibada nje ya msikiti mtakatifu wa Baiti Maqdas wakati wa mfungo wa Ramadhani
Wapalestina wakiandaa eneo la kufanya ibada nje ya msikiti mtakatifu wa Baiti Maqdas wakati wa mfungo wa Ramadhani

Marekani pia imetoa wito wa utulivu, wakati nchi jirani ya Jordan, ambayo inasimamia utunzaji wa maeneo matakatifu ya Waislam Jerusalem, imelaani hatua zilizo chukuliwa na Israeli kulingana na ripoti ya Shirika la Habari la Associated Press.

Jerusalem, ambapo yako maeneo matakatifu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislam, kwa muda mrefu sasa yamekuwa ni kiini cha mgogoro kati ya Israeli na Palestina. Mwaka 2014, mgogoro kama huo ulizuka na vita kuanza iliyodumu kwa siku 50 kati ya Israel na kikundi cha wanamgambo wa Hamas.

Wanawake wa Kipalestina wakisoma Quran nje ya msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa wakati wa sala ya Ijumaa, ikiwa bado janga la corona linaendelea.
Wanawake wa Kipalestina wakisoma Quran nje ya msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa wakati wa sala ya Ijumaa, ikiwa bado janga la corona linaendelea.

Jeshi la Israeli limesema jumla ya roketi 36 zilipigwa kuelekea ndani ya Israeli usiku mzima. Imesema sita kati ya hizo zilizuiliwa, wakati nyingine nyingi ziliangukia katika maeneo yaliyo wazi. Hakuna taarifa za majeruhi au uharibifu mkubwa, lakini roketi hizo zilisababisha ving’ora vya mashambulizi ya angani eneo kote kusini mwa Israeli.

Katika kujibu shambulizi hilo, jeshi limesema ndege za kivita na helicopter zilishambulia maeneo kadhaa ambako Hamas inaendesha shughuli zake huko Gaza, ikiwemo mahandaki na sehemu wanakorushia roketi hizo.

Hamas haijadai kuhusika na ufyatuaji wa roketi hizo, lakini Israeli inaamini kikundi hicho kinahusika na mashambulizi ya roketi yanayotoka katika maeneo hayo.

XS
SM
MD
LG