Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:31

Uingereza na Marekani zaendeleza juhudi za kuimarisha sitisho la mapigano Gaza


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uingereza Dominic Raab.
Chris J Ratcliffe/Pool via REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mwenzake wa Uingereza Dominic Raab. Chris J Ratcliffe/Pool via REUTERS

Juhudi za kidiplomasia za kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza zinaendelea Jumatano. 

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Dominic Raab wa Uingereza wanatembelea nchi za Mashariki ya Kati kujaribu kusitisha kabisa ghasia, kuahidi msaada wa kukarabati Gaza na kuanzisha tena mazungumzo ya Amani.

Waziri Blinken alikutana na Rais Abdel Fatahh al-Sisi mjini Cairo leo akiendelea na juhudi zake za kuimarisha makubaliano yakusitisha mapigano kati ya Israeli na Hamas yaliyosimamiwa na Misri.

Rais Abdel Fattah el-Sissi
Rais Abdel Fattah el-Sissi

Baadae alikutana na Waziri mwenzake Sameh Choukri na Abbas Kamel mkuu wa idara ya ujasusi ya Misri, GIS, maafisa wawili waliokuwa na jukumu kubwa la kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Sameh Shoukrty Waziri wa mambo ya nje wa Misri (kati) wakati wa mkutano na waandishi mjini Ramallah
Sameh Shoukrty Waziri wa mambo ya nje wa Misri (kati) wakati wa mkutano na waandishi mjini Ramallah

Kabla ya kuwasili Cairo Blinken alikutana na Rais Reuven Rivlin na kumkabidhi mualiko kutoka Rais Joe Biden kutembelea Washington.

Wakati wa ziara hii yake ya kwanza Mashariki ya Kati Jumanne mwanadiplomasia mkuu wa Marekani alisema hana mipango ya kufuatilia mazungumzo ya amani kati ya pande mbili kwa hivi sasa.

Lakini alieleza matumaini ya kubuni mazingira bora yatakayopelekea mazungumzo ya amani.

Hata hivyo alisisitiza kwamba Marekani inaunga mkono suluhisho la kundwa kwa mataifa mawili.

Blinken alieleza : "Hatimaye kuna uwezekano wa kuanza tena juhudi za kupatikana suluhisho la mataifa mawili, ambayo tunaendelea kuamini kuwa ndio njia ya dhati kuhakikisha mustakbal wa Israeli kama taifa la Wayahudi na taifa la kidemokrasia na bila shaka kuwapatia Wapalestina taifa wanalostahiki kupata.

Katika kujaribu kufikia malengo hayo Blinken siku ya Jumanne alitangaza kufunguliwa tena ubalozi mdogo wa Marekani kwa ajili ya ushirikiano na Palestina mjini Jerusalem, na kuapa kuimarisha uhisiano na Wapalestina.

Pamoja na kutangaza msaada wa kiuchumi wa dharura wa dola milioni 360 kwa ajili ya kuikarabati Gaza mbali na dola milioni 250 zilizotangazwa mwezi machi. Na alisema serikali ya Washington inajadili na bunge kutoa dola milioni 75 kwa ajili ya huduma za dharura kuwasaidia Wapalestina.

Wapalestina ndani ya hema waloweka juu ya vifusi vya nyumba yao baada ya mapigano kumalizika Gaza
Wapalestina ndani ya hema waloweka juu ya vifusi vya nyumba yao baada ya mapigano kumalizika Gaza

Nayo Misri wiki iliyopita ilitangaza msaada wa dola milioni 500 kuikarabati Gaza.

Mbali na Blinken kutembelea Mashariki ya Kati waziri mwenzake wa Uingereza Dominic Raab alikuwa mjini Jerusalem na Ramalllah Jumatano akihimiza kukomeshwa ghasia za mara kwa mara kupitia suluhisho la mataifa mawili. Huko Jerusalem alikutana na mawaziri wa serikali na baadae kukutana na Rais Mahmoud Abass kwenye Ukingo wa Magharibi.

Rais Mahmoud Abbas
Rais Mahmoud Abbas

Raab alieleza kuwa: "Bila shaka tunataka kuona usitishaji mapigano unaheshimiwa. Tunataka kuisaidia Israeli lakini tunawataka pia Wapalestina wafuate njia kuelekea amani ya kudumu. Huenda ikawa vigumu kwa hivi sasa lakini ni lazima tujitahidi."

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Al-Safadi amekutana na Rais Abass mjini Ramallah kujadili juhudi kuelekea suluhiso la mataifa mawili.

Al-Safadi ameeleza kuwa : "Ikiwa tunataka kuzuia kuzuka tena mapigano na ikiwa tunataka kuhifadhi usitishaji mapigano basi hatunabudi kukabiliana na sababu zinazozusha ugomvi. Hiyo inamaana ya kufanya kazi kumaliza ukaliaji wa ardhi, kupata haki za Wapalestina na kusitisha mashambulio dhidi ya haki za Wapalestina katika maeneo yanayokaliwa ya Jerusalem na msikiti wa al-Aqsa.

Blinken anakutana na Mfalme Abdullah wa Jordan kabla ya kukamilisha ziara yake ya Mashariki ya Kati leo.

XS
SM
MD
LG