Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:14

Ndege za Israeli zafanya mashambulizi mapya Gaza


Kikosi cha Mizinga cha Israeli cha rusha makombora kelekea eneo la Gaza katika mpaka wa Gaza spande wa Israeli Jumamosi, Mei 15, 2021. (AP Photo/Ariel Schalit)
Kikosi cha Mizinga cha Israeli cha rusha makombora kelekea eneo la Gaza katika mpaka wa Gaza spande wa Israeli Jumamosi, Mei 15, 2021. (AP Photo/Ariel Schalit)

Ndege za Israeli zimefanya mashambulizi ya anga huko Gaza mapema Jumamosi na wanamgamnbo wa Hamas wamejibu kwa kufyatua roketi ndani ya Israel.

Wakati huo huo vyanzo vya habari vinaripoti kuwa ghasia kati ya pande hizo mbili zimekuwa zikiendelea kwa usiku ya tano mfululizo.

Shambulizi moja la anga liliua takriban Wapalestina 10 wakiwemo watoto.

Shambulizi jingine limeua watu wawili, maafisa wa afya wa Palestina wamesema.

Mivutano imezidi kuongezeka zaidi hivi leo huku Wapalestina wakiadhimisha siku ya Nakba au siku ya janga, ikiwa ni kumbukumbu ya uharibifu kwenye makazi ya Wapalestina uliofanywa mwaka 1948 kwa kuundwa kwa taifa la Israeli.

Siku ya Ijumaa ghasia zilikuwa kati ya Waisrael na Wapalestina, huku mapigano yakizuka huko Ukingo wa Magharibi pamoja na mashambulizi ya anga huko Gaza.

XS
SM
MD
LG