Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:38

Waziri wa Ulinzi wa Marekani aanza ziara Israeli


 Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin
Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin amewasili nchini Israel Jumapili, ikiwa ni kituo chake cha kwanza katika ziara yake ya siku mbili katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Austin ni kiongozi wa ngazi ya juu katika baraza la mawaziri la Rais Joe Biden kwenda Israel tangu utawala wa Biden utangaze kufanya mazungumzo kufufua makubaliano ya nyuklia yam waka 2015 na Iran.

Waziri Austin anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Israel, Benny Gantz hivi leo.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa mkosoaji mkubwa wa makubaliano ya nyuklia na Iran na kufurahishwa na uamuzi wa Rais wa zamani Donald Trump kuiondoa Marekani katika mkataba huo.

Wiki iliiyopita, Netanyahu amesema kwamba mkataba na Iran, “utafungua njia kwa silaha za nyuklia, silaha ambazo zinatishia uwepo wetu.”

XS
SM
MD
LG