Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:52

Israeli yaendelea kuizuia Iran kufanya mashambulizi


Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu was interviewed Saturday by VOA Persian at the Munich Security Conference in Germany, where he discussed Israel's outreach to Arab countries and the Iran nuclear deal.
Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu was interviewed Saturday by VOA Persian at the Munich Security Conference in Germany, where he discussed Israel's outreach to Arab countries and the Iran nuclear deal.

Mvutano kati ya Israeli na Iran umekuwa unaongezeka kwa haraka katika siku za karibuni wakati vikosi vya Israeli vikiwakabili wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran walioko katika maeneo ya Lebanon na Syria yanayopakana na Israeli.

Wiki hii, mvutano huo uliongezeka zaidi wakati wapiganaji kadhaa – wakiwemo wanamgambo – waliuawa ndege za kivita ambazo hazikutambuliwa ziliposhambulia kituo cha kijeshi cha Syria karibu na mpaka wa Iraqi.

Shambulizi hilo nchini Syria lilitokea wakati vikosi vya Israeli vikiwa katika hali ya tahadhari ya juu katika eneo la kaskazini katika mpaka wao baada ya kuwaua watu wanne wenye silaha waliokuwa wametokea Syria.

Kusudio la Israeli ni kuzima jaribio lolote la Iran kushambulia kwa kutumia mamluki wao nchini Syria na Lebanon.

Jenerali Assaf Orion, Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Usalama anasema : “Tukiangalia mtiririko mzima wa mahitaji ya kijeshi, unaotokana na viwanda vya Iran, hadi Iraq, na mpaka Syria, na Lebanon, Israeli katika miaka ya hivi karibuni ilifanikiwa kuzuia sehemu kubwa ya usambazaji wa silaha hizi, na kurudisha nyuma juhudi za Hezbollah inayosaidiwa na Iran kwa miaka kadhaa.

Mashambulizi ya hivi karibuni nchini Syria yanaongeza mvutano kati ya Israeli na Iran.

Yossi Kuperwasser, Mkurugenzi wa zamani wa Utafiti, Usalama wa Kijeshi IDF : “Kuna mvutano unaoendelea kati ya Israeli na Iran juu ya masuala mawili ambayo ni tofauti kubwa kati ya Israeli na Iran.

Moja, bila shaka, ni mradi wa nyuklia, na jengine ni jaribio la Iran kujenga uwezo wake wa kijeshi karibu na mpaka wa Israeli ili kuishambulia Israeli.

XS
SM
MD
LG