Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:16

Guinea: Rais Conde 82, aidhinishwa kuwania muhula wa 3


Rais wa Guinea Alpha Conde.
Rais wa Guinea Alpha Conde.

Chama kinachotawala nchini Guinea Alhamisi kilimteua rais Alpha Conde kugombea urais kwa mhula wa tatu.

Conde, mwenye umri wa miaka 82, ametumia fursa ya katiba mpya iliyozua utata kugombea tena mhula mwingine madarakani.

Mazungumzo kuhusu uwezekano wake kugombea muhula mwingine madarakani yalisababisha maandamano nchini Guinea, ambayo yamepelekea vifo vya watu 30 kwa mda wa mwaka mmoja sasa.

“Nyote mmezungumza, washirika wetu, vyama na wengine. Nazingatia hilo,” Conde aliwaambia wanachama wa chama chake katika hotuba baada ya kumuidhinisha kugombea urais.

Hata hivyo, hakusema siku ambayo atatangaza rasmi kugombea mhula mwingine.

Conde, ambaye alikuwa mwanasiasa wa upinzani kwa mda wa miaka kadhaa, aliingia madarakani mwaka 2010 baada ya kushinda uchaguzi mkuu.

Waliomchagua walikuwa na matumaini makubwa kwanza angeleta mfumo wa demokrasia nchini humo baada ya utawala wa kidikteta wa miongo kadhaa.

Mwansiasa huyo alishinda mhula wa pili mwaka 2015.

Lakini juhudi zake za kusalia madarakani zimesababisha wasiwasi kwamba huenda Guinea ikafuata mkondo wa nchi zingine za Afrika ambazo viongozi wake wamekataa kuondoka madarakani baada ya mda wao kumalizika.

Wafuasi wake Conde wanasema kwamba mabadiliko ya katiba ya mwezi Machi kupitia kura ya maombi ambayo ilisusiwa na vyama vya upinzani, yalitoa fursa kwa kiongozi huyo kugombea mihula miwili upya.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG