Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 16:18

Membe na Maalim Seif kugombea urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo


Seif Sharif
Seif Sharif

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, chama cha ACT Wazalendo kimewapitisha Bernard Membe na Seif Sharif Hamad kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya chama hiko.

Katika mkutano mkuu wa chama hiko uliofanyika Jumatano jijini Dar es salaam pia umepitisha Ilani ya chama hiko ambapo miongoni mwa masuala yanayoanisnwa ni Kujenga Uchumi Jumuishi unaobeba maendeleo ya watu na si vitu pekee

Pia salamu za pongezi zilimimika kutoka kwa vyama washirika kwa wateule Bernard Membe na Maalim Seif Sharif Hamad watakonadi Ilani ya uchaguzi ya ACT wazalendo na kuwashawishi Wananchi kuwapa mamlaka ya juu ya Tanzania, lakini sikisisitiza kuwepo uchaguzi huru na haki.

Tundu Lissu ambaye ni Mgombea wa nafasi ya Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA alivitaka vyama vya upinzani katika ujumbe wake katika mkutano huo ni lazima upinzani uwe na kauli moja.

Msajili wa vyama vya siasa kama mlezi wa vyama hivi amevitaka vyama vyote vya siasa kuheshimu taratibu na sheria za uchaguzi.

Wakati huohuo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeatangaza kuanza kwa shughuli ya uchukuaji fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia wiki hii na tayari baadhi ya vyama vimetoa ratiba ikiwemo Chama cha Mapinduzi ambapo mgombea wao Rais John Magufuli anataraji kuchukua fomu hizo wiki hii.

XS
SM
MD
LG