Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:05

Viongozi wa dunia watuma rambirambi Lebanon huku juhudi za uokozi zikiendelea


Majeruhi akisaidiwa kuondoka katika eneo la tukio la mlipuko mjini Beirut, Lebanon Agosti 4, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir
Majeruhi akisaidiwa kuondoka katika eneo la tukio la mlipuko mjini Beirut, Lebanon Agosti 4, 2020. REUTERS/Mohamed Azakir

Maafisa wa serikali ya Lebaon Jumatano wamesema huenda idadi ya vifo kutokana na mlipuko mkubwa kabisa kuwahi kutokea katika jiji la Beirut ikaongezeka kwa sababu operesheni ya kuwatafuta watu chini ya vifusi vya majengo yalioharibika bado inaendelea.

Hata hivyo kilichosababisha mlipuko huo bado hakijafahamika, lakini maafisa wa serikali wanadhani ni kutokana na tani 2,700 za kemikali ya kutengeneza mbolea na bomu aina ya ammonium nitrate zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya ghala bandarini katikati ya mji kwa muda wa miaka 6 iliopita.

Viongozi wameomba kufanyike uchunguzi wa haraka, huku Waziri Mkuu Hassan Diab akiahidi kuwa waliohusika na mlipuko huo watachukuliwa hatua kali.

“ Kilichotokea leo hakitapita bila uwajibikaji, wale ambao walihusika watapewa malipizi ya kilichotokea, hii ni ahadi kwa wahanga na waliojeruhiwa, hii ni ahadi ya kitaifa. Ukweli utawekwa wazi juu ya ghala hili hatari ambalo limekuepo tangu mwaka wa 2014,” amesema waziri mkuu Diab.

Baada ya mlipuko huo mkubwa uliotokea Jumanne jioni, watu wengi walionekana wakikimbilia hospitali kutafuta huduma za afya.

Ubalozi wa Marekani mjini Beirut uliomba watu kubaki ndani ya nyumba zao baada ya ripoti kuwa kuna gesi zenye sumu hewani kutokana na mlipuko huo.

Rais Michel Aou ambae leo ameitisha kikao cha dharura cha baraza lake la mawaziri, amesema wahusika watapewa adhabu kali sana. Pia yeye na waziri mkuu walitembelea bandari ya Beirut ambako mlipuko ulitokea na kusema

“Haikubaliki kuwa shehena ya tani 2000 na nyingine tani 750 za kemikali ya ammonium nitrate kuhifadhiwa katika ghala kwa miaka 6, bila kuchukua hatua za kuzuia ambazo zinahatarisha usalama wa raia”, Aoun ameandika kwenye twitter.

Jumuia ya kimataifa imetoa rambi rambi kutokana na vifo vilivyotokea na imeahidi kuwasaidia watu wa mjini Beirut.

Papa Francis alikuwa miongoni wa viongozi wa dunia aliyotoa ujumbe akiitka jumuia ya kimataifa kuiombea Lebanon na wakazi wake.

Papa Francis :”Tuwaombe aathiriwa na familia zao na tuiombe lebanon ili kwa dhamira yetu sote, walebanon waweze kukabiliana na janga hili kwa upande wa kijamii, kisiasa na kidini. Na kwa msaada wa jumuia ya kimataifa waweze pia kutanzua hali ngumu inayowakabili kwa hivi sasa.”

Qatar tayari imepeleka Hospitali ya muda Jumanne kuwasaidia walojeruhiwa.

Rais wa Marekani Donald Trump akizungumza jana na waandishi habari amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Lebanon.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake itatuma madaktari wa dharura na tani kadhaa za vifaa vya matibabu, huku Russia ikisema itachangia katika ujenzi wa hospitali ya dharura na kutuma madaktari.

Jordan nayo imesema itatuma madaktari wake mjini Lebanon, naye rais wa Iran Hassan Rouhani amesema serikali yake itatuma msaada wa vifaa vya matibabu.

Umoja wa Mataifa nao umesema uko tayari kusaidia wananchi wa Lebanon katika wakati huu mgumu.

Makamo rais wa zamani ambaye atashindana na Trump kwenye uchaguzi ujao wa Novemba, Joe Biden amewapa pole waathirika na ameomba utawala wa Trump na jumuia ya kimataifa kukusanya haraka msaada wa dharura, kwa ajili ya maelfu ya watu waliojeruhiwa katika mlipuko huo.

XS
SM
MD
LG