Ushirikiano huo wa kihistoria umeelezwa na Washington kuwa umehamasisha ushirika dhidi ya Iran na uwezekano wa kupanua nyanja za kiuchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, Abdullatif Al-Zayani aliongoza ujumbe ambao ulisafiri kwa ndege ya shirika la ndege la Gulf kwenda Tel Aviv ikiwa ni ndege ya kwanza ya abiria.
Akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israeli Gabi Ashkenazi kwenye uwanja ndege, Al-Zayani alitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo mjini Jerusalem.
Mkurugenzi Mkuu katika Wizara ya Mambo ya nje ya Israel Alon Ushpiz ameiambia radio ya Israel kwamba maafisa watasonga mbele kutekeleza waraka wa maelewano uliotiwa saini mwezi October mjini Manama ambao unahusu usafiri wa anga, visaz na ufunguzi wa ofisi za kibalozi.