Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:06

Israeli na UAE wakubaliana kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia


Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza Alhamisi kuwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Israeli wamekubali kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia.

Tangazo hili linaifanya UAE kuwa nchi ya tatu ya Kiarabu na taifa la kwanza la Ghuba ya Kiarabu kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Israeli. Misri na Jordan ni nchi pekee zilizokuwa na mahusiano na Israeli.

Trump aliandika katika ujumbe wa twitter kuhusu tamko la pamoja kati ya nchi hizo tatu, akisema kuwa hilo, “kwa kweli ni jambo la kihistoria.”

Tamko hilo la pamoja limesema kuwa wajumbe watakutana katika wiki zijazo kujadili na kusaini makubaliano ya safari za moja kwa moja za ndege, usalama, mawasiliano, nishati, utalii na huduma za afya.

UAE na Israeli pia zinapanga “kupanua nakuchochea ushirikiano katika tiba na utengenezaji wa chanjo ya virusi vya corona..”

Trump aliongeza kuwa,” ilivyokuwa hivi sasa makubaliano yamefikiwa natarajia mataifa ya Kiarabu na Kiislam yatafuata mfano wa UAE.”

XS
SM
MD
LG