Jeshi limesema kwamba mashambulizi yanaendelea kushinda nguvu wapiganaji hao wanaotumia wakaazi wa sehemu hiyo kama kinga, shirika la habari la kimataifa AFP limeripoti Alhamisi.
Makabiliano yameripotiwa katika siku chache zilizopita kati ya wanajeshi wa serikali na kundi la wapiganaji katika bandari, kaskazini mwa Msumbiji ambako kuna utajiri wa gesi.
Katika miezi ya hivi karibuni, kundi la wapiganaji linaloripotiwa kuwa na uhusiani na kundi la Islamic state limeteka nyara miji kadhaa na kusababisha maelfu ya watu kutoroka makwao.
Tanzania imesema kwamba itaanza mashambulizi dhidi ya wapiganaji hao katika msitu unaopakana na Msumbiji.