Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:25

Zoezi la kunyang'anya silaha raia Sudan Kusini lauwa 81


 Sudan Kusini
Sudan Kusini

Mamlaka nchini Sudan Kusini zinaeleza takriban watu 81 wameuawa katika mapambano makali baina ya kundi la raia wenye silaha na wanajeshi waliokuwa katika zoezi la kunyang’anya silaha.

Wakati bunduki na silaha nyingine zikiwa bado mikononi mwa raia, na hivyo suala hilo kuwa changamoto kubwa kwa serikali kuwanyang'anya raia ambao wanadai kuwa wanamiliki kwa ajili ya kujihami.

Milioni kadhaa za silaha zinazokadiriwa kuwa mikononi mwa raia na kuendelea kwa mapambano ya silaha baina ya makundi ya kijamii kinzani, kuwanyang'anya silaha wananchi ni changamoto kubwa inayoikabili serikali ya umoja wa kitaifa.

Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa iliundwa mapema mwaka huu baada ya kufikia muwafaka kumaliza vita vya wenye kwa wenye nchini Sudan Kusini iliyodumu kwa miaka sita.

Msemaji wa Jeshi la taifa la Sudan Kusini amesema viajan wenye silaha walishambulia kombi ya jeshi siku mara mbili.

Mapambano kati ya pande mbili yaliendelea kwa saa nyingi. Kati ya wale waliouawa ni wanajeshi 55.

XS
SM
MD
LG