Milipuko hiyo ilisababisha vifo vya takriban watu 160 na Zaidi ya elfu tano kujeruhiwa.
Waandamanaji hao wamekuwa pia wakitaka serikali ya Diab kujiuzulu, kwa shutuma za uongozi mbaya na kuhujumu uchumi wa nchi hiyo.
Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini humo, Diab alisema amechukua hatua hiyo ili kutoa nafasi ya "kuokoa Lebanon," na kuongeza kwamba raia wa nchi hiyo watashiriki katika mchakato huo.
"Mungu isaidie Lebanon," alisema.
Diab aliunde serikali mwezi Januari mwaka huu, baada ya vuta nikuvute ya kisiasa, ambayo hata kabla ya hapo, mara kwa mara ilikuwa ikishuhudiwa nchini humo.
Kabla ya tangazo la kujiuzulu kwa utawala wake Jumatatu, mawaziri na wabunge kadhaa tayari walikuwa wamejiuzulu.
Makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa kulinda usalama yamekuwa yakishuhudiwa tangu Jumamosi.
Milipuko ya Jumanne, ambayo inadaiwa kusababishwa na kemikali aina ya Ammonium Nitrate, inakadiriwa kusababisha hasara ya takriban dola billion tano za Marekani.